Antoni wa Padua


Mt. Fransisko wa Asizi na mfuasi wake Mt. Antoni wa Padua katika mchoro wa Simone Martini

Njozi ya Mt. Antoni wa Paduailivyochorwa na Gaetano Lapis

Basilika la Mt. Antoni wa Padua
Antoni wa Padua, kwa jina la kiraia Fernando Martim de Bulhões e Taveira Azevedo (LisbonUreno 15 Agosti 1195 - PadovaItalia 13 Juni 1231) alikuwa padri na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, maarufu hasa kwa mahubiri yake yaliyomstahilia heshima ya kutangazwa Mwalimu wa Kanisa.
Kwa vipawa vyake vya pekee upande wa akilielimubusarakiasiari ya kitume na sala hasa, alichangia sana maendeleo ya shirika lake.
Ni mmojawapo kati ya watakatifu wanaoheshimiwa zaidi katika Kanisa Katoliki, pia kwa sababu ya miujiza mingi inayosemekana kupatikana kwa kukimbilia maombezi yake.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Juni.
Waamini wengi wanapenda picha zinazomuonyesha akiwa na maua meupe pe, yakimaanisha usafi wa moyo wake, na akimshika mtoto Yesu mikononi, kadiri ya tukio la ajabu lililosimuliwa na vyanzo mbalimbali.

1 maoni:

  1. Mt Antony wa Padua naomba njibiwa barua yangu ya marekebisho ya malipo ya uhamisho wangu ili nilipwe kihalali kama wenzangu Amen

    JibuFuta

 
Top